
Sherehe hii iliandaliwa na Taasis ya Harakati ya Qur’ani Tukufu kama sehemu ya toleo la nane la Mpango wa Kitaifa wa Kuhifadhi Qur’ani , ambao unafanyika chini ya usimamizi wa taasisi hiyo.
Mchango wa Qur’ani Tukufu Katika Taifa la Algeria
Katika hotuba yake kwenye sherehe hiyo, Sheikh Muhammad Ma’mun Qassemi al-Hassani, msimamizi wa Msikiti Mkuu wa Algiers, alisema kuwa Qur’ani Tukufu imekuwa na inaendelea kuwa rejea muhimu katika maisha ya taifa la Algeria na chanzo cha hamasa kwa wapigania uhuru wa Algeria wakati wa harakati za ukombozi wa nchi hiyo.
Alisema kwamba ulinzi na uimara wa taifa umetokana na mafundisho ya Qur’ani, ambayo ndio msingi wa nguvu na uthabiti wake.
Al-Hassani aliongeza kuwa Quran imekuwa mwongozo wa elimu na maadili kwa vizazi mbalimbali nchini Algeria, na akasisitiza kuwa:
"Tunapaswa kubaki waaminifu kwa ujumbe wa Qur’ani, kama walivyokuwa mababu zetu."
Umuhimu wa Kuhifadhi Qur’ani Tukufu na Kuwekeza kwa Vijana
Aidha, alisisitiza kuwa jukumu la Taasisi ya Harakati ya Quran katika jamii ya Algeria ni pana, kwani kujadili ujumbe wa Qur’ani Tukufu nchini humo kunamaanisha kuzungumzia harakati kubwa na shirikishi ya kusoma Qur’ani Tukufu.
Pia alielezea kuwa kuwaheshimu wahifadhi 500 wa Qur’ani ni tukio la kihistoria, linaloonyesha umuhimu wa kuwekeza kwa vijana, ambao ndio msingi wa mustakabali wa Algeria.
Programu ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur’ani Tukufu
Miongoni mwa wazungumzaji wengine katika hafla hiyo alikuwa Ibrahim Lamouri, rais wa taasisi hiyo nchini Algeria.
Alisema kuwa toleo la nane la mpango wa kitaifa wa kuhifadhi Qur’ani nchini Algeria limefanyika kama sehemu ya juhudi kubwa kupitia kambi za kuhifadhi Qur’ani Tukufu zinazoendeshwa na taasisi hiyo.
Aliongeza kuwa mpango huu unahusisha majimbo yote ya Algeria na umewavutia maelfu ya watu wa makundi mbalimbali ya umri.